Wednesday, August 15, 2012

mwanzo mgumu


Mimi ninaitwa PATRICK MPOGOLE nimezaliwa Dodoma mwaka 1979 december5
kabila langu ni mhehe, Dodoma wakati wazazi walikua kikazi kwa muda lakini nyumbani kwetu ni
IRINGA, Nilikulia mkoa huu
Katika maisha ya wazazi yalikua hatarini huko Dodoma sababu  baba yangu alikua na kazi ya polisi
hivyo alifanya kazi kwa bidii sana mara ya mwisho alikamata wamasai kwa wizi wa ng'ombe wengi
na kuwafikisha vyombo vya sheria, Hivyo ilichoendelea serikali haikumpa baba ulinzi wa kutosha
matokeo yake wamasai wakampa vitisho vya hali ya juu
Wazazi wangu wakakimbia kabisa Dodoma na kurudi Iringa kwao na kuanza upya maisha na elimu ya ualimu wakati baba anasoma na mimi nikaanza shule ya msingi na nilipofikia darasa la tatu baba alipata kazi mpya ya ualimu hapohapo na mimi niliugua homa kali
Na baada ya kupona nilipatwa na ulemavu wa kutosikia Wazazi wakanipeleka DSM kwa matibabu,
hospital nilitoroka sababu walitaka nifanyiwe upasuaji pasipo uchunguzi wa kitaalamu, Hivyo baba alinikubai nilipotoroka sababu hakua na uwezo kifedha .Baba akaamua kunipeleka shule ya viziwi DSM na kuniacha nikiendelea na masomo pia nilikua nafanya vizuri sana kila somo na kila kazi pamoja na sanaa mbalimbali kama vile uchoraji na muziki mpaka walimu walinishangaa sana na kunitumaa kama chombo cha kufundishia wanafunzi wengine,
 Wakati wa likizo nilikua nabaki shule na walezi wa shule sababu ya kukosa nauli pamoja na mawasiliano na wazazi, Nilipomaliza shule nilifaulu kuingia elimu ya sekondari pia nilisoma kwa shida sababu ni shule ya mchanganyiko viziwi na wazima, walimu walikua wanafundisha vizuri wazima
Nilimaliza elimu ya sekondari na nilifeli sababu ya ukosefu wa walimu wa kufundisha viziwi.
Sikukata tamaa katika elimu na maisha nikaanza kujishugulisha na vibarua vya kazi ya sanaa kwa kua nilikua na vipaji vingi sana,mpaka nikaitwa hapa NEEMA C. Kuwa kama mwalimu wa sanaa za batik na printing,
Katika maisha ya sasa Naishi kwa kutegemea sanaa, nafanya kazi za sanaa mbalimbali,
FAMILIA, nina familia pia familia yangu mahitaji yote inategemea kipato kitokanacho na vipaji vya sanaa
Pia nimesomesha na bado nasomesha shule wadogo zangu na ndugu zangu yatima
MALENGO MAKUU NILIYOPANGA;
Mwaka 2015 kuwa na kituo maalumu kinaitwa KUKAYE AFRICA HOUSE OF ARTS AND SCHOOL OF ARTS kituo hiki kitatoa mafunzo ya sanaa na ajira kwa vijana wasio na uwezo ila wenye vipaji katika sanaa, Sanaa zitakazokuwapo ' Africa music,fashion designs, and colour designs
          HUDUMA ZITAKAZOKUWAPO
Camp sites and africa hoster, KARIBUNI  sana wote
    Kwa yeyote anaependa kushirikiana namimi anakaribishwa sana kwa amani na upendo


                                                                                                                                                      

No comments:

Post a Comment